Skip to main content
All CollectionsApplication za Pendwa
Jinsi ya ku-download filamu na tamthilia
Jinsi ya ku-download filamu na tamthilia

How to download movies and episodes on Pendwa (Swahili instructions).

J
Written by Jovin Mwilanga
Updated over a week ago

Habari na karibu Pendwa. Tumekuwekea maelekezo hapo chini.

Kama unatumia simu ya Android (Samsung, Infinix, Tecno n.k)

Kwa sasa hivi, tunafanya kazi kwa bidii ili kukuletea application yetu rasmi ya Pendwa ili uweze kuipakua moja kwa moja kwenye simu yako kutoka Play Store. Tutatangaza pale itakapokuwa tayari. Application hii ndio itakayo kuruhusu ku-download filamu na sehemu za tamthilia.

Kama unatumia simu ya iPhone au iPad

Unaweza kupakuwa application yetu hapa https://apps.apple.com/us/app/pendwa/id1583385146. Application hii itakuruhusu ku-download filamu na tamthilia ili uweze kuziangalia baadae hata bila intaneti.

Jinsi ya ku-download kwenye iPhone

  1. Hakikisha umeshamaliza kutengeneza akaunti yako ya Pendwa.


  2. Hakikisha filamu au tamthilia unayotaka kudownload tayari umeshaikodi au kuinunua.


  3. Kwa filamu bonyeza kitufe chenye alama ya ku-download ⬇ kilichopo upande wa kulia ili uanze ku-download filamu hiyo.


  4. Kwa tamthilia, nenda kwenye sehemu (episode) ya tamthilia hiyo kisha bonyeza kitufe chenye alama ya ku-download ⬇ kilichopo upande wa kulia ili uanze ku-download filamu hiyo.


  5. Ili kuona filamu au tamthilia ambazo tayaru umeshazi-download, unaweza kugusa kitufe kilichoandikwa "Downloads" chini kabisa kwenye simu yako. Baada ya hapo, utaweza kuona filamu na tamthilia zako zote hata ukiwa hauna intaneti.

Did this answer your question?