All Collections
Kulipia filamu na tamthilia
Kulipia kwa simu kwenye Android (Samsung, Infinix, Tecno n.k.)
Kulipia kwa simu kwenye Android (Samsung, Infinix, Tecno n.k.)

How to pay for movies and TV shows via mobile money on your Android device (Swahili instructions).

J
Written by Jovin Mwilanga
Updated over a week ago

Melekezo yafuatayo yatakuonyesha jinsi ya kulipia kwa simu kwenye simu yako yenye mfumo wa Android.

Filamu na sehemu za tamthilia kadhaa hapa Pendwa ni bure. Ushauri wetu ni kuchagua filamu au tamthilia unayotaka kuangalia na kama itahitaji kulipiwa, basi utapewa maelekezo yote.

  1. Hakikisha upo kwenye ukurasa wa filamu au tamthilia unayotaka kuangalia. Kama bado wewe ni mgeni hapa Pendwa, basi angalia maelekezo ya jinsi ya kuniunga na Pendwa hapa



  2. Kama ni filamu basi utagusa kitufe kilichoandikwa "Play" au "Resume". Kama ni tamthilia basi utagusa kwenye kitufe kilichoandikwa "Play" au "Resume". Kama umeshaanza kuitazama tamthilia yako, unaweza ukaenda chini kidogo ili kuchagua msimu (season) na sehemu (episode) unayotaka kuangalia.

  3. Kama filamu au sehemu hiyo ya tamthilia itaanza ku-play, basi filamu au sehemu hiyo haihitaji malipo au tayari umeshailipia.

  4. Kama ukurasa ufuatao ukifunguka, basi itabidi utumie vocha zako kukodi au kununua filamu au sehemu hiyo ya tamthilia.




  5. Tukitumia mfano hapo juu, kukodi kipindi hiki kunagharimu vocha 0.25. Kama vocha ulizonazo zaidi ya 0.25 basi unaweza kukodi. Kama vocha ulizonazo ni chini ya 0.25, basi itabidi ununue vocha za ziada ili uongeze salio kwenye akaunti yako.

  6. Pitia chaguo mbalimbali kwenye ukurasa huo na pale utakapokuwa tayari, basi utagusa "Kodi kipindi" au "Kodi Msimu" n.k.


  7. Kwenye ukurasa huu, utachangua "Ongeza kwa simu". Chaguo hili litakupa maelekezo yote ya kulipia kwa simu.


  8. Maelekezo hayo yatakuonyesha jinsi ya kuongeza vocha kwa kutuma malipo kwenda kwa wakala wetu. Wakala wetu akipata malipo, atakutumia namba ya vocha yako moja kwa moja kuja kwenye simu yako. (Wakala atatuma namba ya vocha hiyo kuja kwenye namba ya simu iliyotuma malipo)



  9. Ukipata namba ya vocha yako basi utaweka kwenye sanduku lililoandikwa "Namba/Herufi za vocha". Baada ya hapo, utagusa kitufe kilichoandikwa "Weka Vocha".

  10. Sasa akaunti yako itakuwa na vocha za kutosha kukodi au kununua filamu na sehemu za tamthilia hapa Pendwa.

Unaweza pia kutumia ukurasa huu https://www.pendwa.app/voucher kupata maelekezo ya kutuma malipo na kuongeza salio kwenye akaunti yako.





Did this answer your question?