All Collections
Kulipia filamu na tamthilia
Kulipia kwa simu kwenye iPhone/iPad
Kulipia kwa simu kwenye iPhone/iPad

How to pay for movies and TV shows via mobile money on your iPhone or iPad (Swahili instructions).

J
Written by Jovin Mwilanga
Updated over a week ago

Melekezo yafuatayo yatakuonyesha jinsi ya kulipia kwa simu kwenye iPhone au iPad.

Filamu na sehemu za tamthilia kadhaa hapa Pendwa ni bure. Ushauri wetu ni kuchagua filamu au tamthilia unayotaka kuangalia na kama itahitaji kulipiwa, basi utapewa maelekezo yote.

  1. Hakikisha upo kwenye ukurasa wa filamu au tamthilia unayotaka kuangalia. Kama bado wewe ni mgeni hapa Pendwa, basi angalia maelekezo ya jinsi ya kuniunga na Pendwa hapa



  2. Kama ni filamu basi utagusa kitufe kilichoandikwa "Play" au "Resume". Kama ni tamthilia basi utagusa kwenye kitufe kilichoandikwa "Play" au "Resume". Kama umeshaanza kuitazama tamthilia yako, unaweza ukaenda chini kidogo ili kuchagua msimu (season) na sehemu (episode) unayotaka kuangalia.

  3. Kama filamu au sehemu hiyo ya tamthilia itaanza ku-play, basi filamu au sehemu hiyo haihitaji malipo au tayari umeshailipia.

  4. Kama ukurasa ufuatao ukifunguka, basi itabidi ukodi au ununue filamu au sehemu hiyo ya tamthilia.


  5. Changua kati ya kukodi (rent) au kununua (buy/purchase). Kukodi mara nyingi kunagharimu vocha (credits) chache ukilinganisha na kununua. Tukitumia mfano hapo juu, kukodi kipindi hiki kunagharimu vocha 0.25. Kama vocha ulizonazo zaidi ya 0.25 basi unaweza kukodi. Kama vocha ulizonazo ni chini ya 0.25, basi itabidi ununue vocha za ziada ili uongeze salio kwenye akaunti yako. Gusa chaguo lako.



  6. Kama una vocha za kutosha, basi utaweza kukodi au kunua kwa kugusa kilichoandikwa "Rent" au "Buy". Kama huna vocha za kutosha, utagusa kitufe kilichoandikwa "Not enough credits. Add credits" ili kuongeza salio.


  7. Kwenye ukurasa huu, utachangua "In Tanzania?" "Pay by Mobile Money". Chaguo hili litakupeleka kwenye ukurasa wa kuongeza salio kwa kutuma malipo.


  8. Utatumia kitufe "Sign in to Apply Voucher" ili kuingia kwenye akaunti yako.


  9. Maelekezo hayo yatakuonyesha jinsi ya kuongeza vocha kwa kutuma malipo kwenda kwa wakala wetu. Wakala wetu akipata malipo, atakutumia namba ya vocha yako moja kwa moja kuja kwenye simu yako. (Wakala atatuma namba ya vocha hiyo kuja kwenye namba ya simu iliyotuma malipo)



  10. Ukipata namba ya vocha yako basi utaweka kwenye sanduku lililoandikwa "Namba/Herufi za vocha". Baada ya hapo, utagusa kitufe kilichoandikwa "Weka Vocha".

  11. Sasa akaunti yako itakuwa na vocha za kutosha kukodi au kununua filamu na sehemu za tamthilia hapa Pendwa.

  12. Rudi kwenye application ya Pendwa.


  13. Kama bado kitufe hapo chini kinasema "Not enough credits. Add Credits", basi utagusa kitufe hapo juu kilichoandikwa "Refresh".

Unaweza pia kutumia ukurasa huu https://www.pendwa.app/voucher kupata maelekezo ya kutuma malipo na kuongeza salio kwenye akaunti yako.

Did this answer your question?