All Collections
Gharama za Pendwa
Gharama za kutumia Pendwa
Gharama za kutumia Pendwa

Learn more about what it costs to use Pendwa (Swahili instructions)

J
Written by Jovin Mwilanga
Updated over a week ago

Pendwa ni platform ya kuangalia filamu na tamthilia za Kiswahili.

Kama platform zingine kwenye intaneti, unahitaji kuwa na intaneti (bando, salio n.k.) ili uweze kujiunga au kuangalia filamu na tamthilia hapa Pendwa.

Gharama za kujiunga

Kujiunga na Pendwa ni bure kabisa. Kama bado hujajiunga na Pendwa basi tumekuwekea maelekezo hapa:

Gharama za kuangalia

Baadhi ya filamu na sehemu za tamthilia hapa Pendwa ni bure. Filamu na sehemu za tamthilia ambazo ni bure huwa zinabadilishwa kila wiki.

Filamu na sehemu za tamthilia nyingine zinahitaji kulipiwa. Bei zetu zinatokana na filamu au tamthilia yenyewe. Ushauri wetu ni uingie kwenye platform yetu na utafute filamu au tamthilia unayotaka kuangalia. Kama utahitaji kulipia basi utapelekwa moja kwa moja kupata maelekezo yote kwenye ukurasa wa kulipia filamu au sehemu ya tamthilia hiyo.

Muongozo zaidi

Did this answer your question?